Stoku
Namba za Serial na Dhamana
Namba ya serial (au IMEI) kwa kila kipande: imepokelewa lini, imeuzwa kwa nani, dhamana na historia yake.
Ilisasishwa 29 Okt 2026
Washa Namba za Serial kwenye Wasifu wa Kampuni → Vipengele. Kisha, kwenye bidhaa, chagua Kila kipande kina namba ya serial na weka Dhamana (miezi).
Zinaulizwa lini
- Zinazoingia: bidhaa za oda ya manunuzi zikipokelewa, andika au skani namba moja kwa kila kipande. Kwa vipande vilivyopo tayari stoku, tumia Namba za Serial → Ongeza kwenye Stoku.
- Zinazotoka: mauzo yakichukuliwa, chagua namba zilizochukuliwa. Mauzo yaliyofanyika kaunta yanapata namba zake kwenye ukurasa wa mauzo (Weka kwenye Mauzo). Dhamana inaanza siku ya mauzo.
- Uhamisho: weka namba za vipande vinavyotumwa. Upande wa pili, chagua vilivyofika.
Kama bidhaa ina namba chache stoku kuliko idadi yake (stoku ya zamani bila namba), namba hizo tu ndizo zinaulizwa.
Tafuta moja
Skani au andika namba ya serial kwenye Namba za Serial (au kwenye Skana): unaona bidhaa, iko wapi, manunuzi iliyokuja nayo, mteja aliyeinunua, dhamana, na kila hatua ya historia yake.
Kubadilisha moja kwa mkono
Kwenye ukurasa wake: Imefutwa (imepotea, imevunjika), Imerudishwa kwa msambazaji, au Imerudi stoku (imerudishwa). Hii inabadilisha namba tu; badilisha stoku yenyewe kwa marejesho, kuondoa stoku au kuhesabu.
Mauzo yakibatilishwa, namba zake za serial zinarudi stoku.
